Tuesday, July 7, 2020

VYAKULA AMBAVYO HUPASWI KULA MARA KWA MARA

Linapokuja suala la kula. Ulimi hupenda vitu vitamu vitamu.
Mzee tumbo wala hanaga shida. Husema ameshiba. Bila ya kujali umekula nini.
Shida iko katika moyo. Kukubali kuridhika kwa kile ulichojaaliwa kukipata. Ili mkono uende kinywani.
Kula vizuri ni suala zuri. Cha kujiuliza ni je, ninachokula ni chema kiafya? Kina madhara gani mwilini? Kinanifanya nijisikieje? Je nakunya vizuri?
Leo nita — share vyakula kumi. Ambavyo hupaswi kula. Hata ukishauriwa na Bwana Daktari. Navyo ni pamoja na:

Nafaka Zilizokobolewa

Tukianza na mchele uliokobolewa. Mchele huu haufai kiafya. Kwa sababu ukoboaji unafanya virutubishi kuondolewa. Pia nyuzi nyuzi huondolewa. Mchele huu mweupe unaweza kukufanya upate matatizo ya mmeng’enyo wa chakula tumboni. Pia ulaji wa mchele huu haukupi lishe yeyote zaidi ya kujaza tumbo. Badala yake unapaswa kula mchele wa kahawia. Mchele huu una madini mengi na vitamini kwa ajili ya afya yako.
Pia sembe haifai kwa afya yako. Kama mchele. Ukoboaji wa mahindi kupitiliza unayafanya yapoteze madini na vitamini. Pamoja na wanga. Ambavyo ni vitu muhimu kwa kuutia mwili nguvu na afya. Badala yake unga wa dona ndio unafaa kiafya. Kwa sababu mahindi yanasagwa yakiwa na ganda lake. Pia kiini hakiondolewi ambacho ndio ‘target’ ya panya mharibifu.
Bila kusahau ngano iliyokobolewa pia haifai. Waweza kusema mbona unga huu unaongezewa vitamini na madini kiwandani? Chakula bora hakipatikani kiwandani. Wala hakihitaji kuongezewa virutubishi.

Mkate Mweupe

Mkate huu ni zao la ngano iliyokobolewa. Hivo haufai kabisa kiafya kama tulivyoona kuwa, ngano iliyokobolewa imeondolewa virutubishi. Badala yake kula mkate wa kahawia. Unaotokana na ngano isiyokobolewa.

Juisi za Matunda

Ndiyo. Juisi za matunda. Hapa sizungumzii juisi zile za kiwandani. Ambazo zimewekwa ladha tu ya matunda lakini hazina uhalisia wowote. Nazungumzia juisi ile unayoitengeneza nyumbani. Inasemekana kuwa juisi hiyo ina sukari vijiko kumi sawa na chupa ya soda. Haifai kiafya. Unapotengeneza juisi kwa kusaga matunda una haribu nyuzi nyuzi zilizokatika matunda. Hivyo ikiwa una matatizo ya mmeng’enyo wa chakula. Ni afadhali ule matunda kama yalivyo. Badala ya kunywa juisi yake.

Soda

Kama nilivyoeleza hapo juu. Soda ina vijiko kumi vya sukari. Sukari inapozidi mwilini, kongosho inashindwa kupambana na sukari hii. Hivyo kusababisha ugonjwa wa kisukari.
Rangi inayoongezwa kenye soda inaaminika kusababisha saratani ya mapafu na ini.
Vile vile soda kwa watoto wandogo huongeza hatari ya kunenepa kupindukia.
Pia soda inakufanya uishiwe maji mwilini.
Badala yake kunywa maji mengi. Ikiwa hupendi ladha ya maji. Yachanganye na vipande vya limao kwa manufaa zaidi.

Chipsi

Chakula cha fasta au siyo. Chakula pendwa cha akina dada. Lakini hata wanaume! Wengi wetu tunakula chipsi. Hii ni kutokana na uvivu wa kupika au sababu zingine.
Hupaswi kula chipsi kwa sababu zina mafuta mengi. Vyakula vilivokaangizwa vina mchango mkubwa katika kusababisha kutopata choo. Au kupata choo kama cha mbuzi.

Tambi

Tambi zinatengenezwa kwa ngano iliyokobolewa. Kwa hiyo haina virutubisho vyovyote. Licha ya kuongezewa viungo kama vitamini, mafuta na madini. Hivi vyote ni takataka ambazo hazifai kuingia mwilini.

Mafuta ya Kupikia ya Kiwandani

Imekuwa kibiashara sana siku hizi. Baada ya kuona kuwa watu wanapata ufahamu zaidi kuhusu vyakula. Utaona kibandiko ‘Hayana Lehemu’. Au ‘Mafuta Asili’. Mamlaka za chakula na dawa huweza kutoa ruhusa ya wazalishaji kuweka vibandiko hivyo ikiwa tu wamekidhi viwango fulani. Hii haimaanishi kuwa ni kweli mafuta hayo ya kupikia hayana lehemu. Badala yake kula mafuta ya alizeti, karanga n.k. Yaliyochujwa kwa mashine za mtaani. Na kuuzwa yakiwa ‘pure’ bila kuchanganywa na kitu kingine chochote.

Maandazi

Unapopika chakula kwa joto jingi kupita kiasi. Chakula hicho kinapoteza virutubishi na kugeuka ‘garbage’ ama ‘junk’. Maandazi huivia mafuta yenye joto kali sana. Pia kwa kuwa yanaivia mafuta, hii ina maana kwamba maandazi yana mafuta mengi. Ambayo huweza kusababisha matatizo ya mmeng’enyo wa chakula pamoja na unene. Pia hayana virutubisho vya asili kwa kuwa yanatengenezwa kwa ngano iliyokobolewa. Ingawa kuna maandazi ya ngano isiyokobolewa, lakini kitendo cha kuyapika kwa mafuta yenye joto kupita kiasi. Kunayafanya nayo pia yakose lishe bora kiafya.

Chumvi Ya Mezani

Utaambiwa imeongezwa madini ya joto. Lakini chumvi hii ya mezani katika uasili wake siyo nyeupe kama unavyoiona. Inachimbwa na ku — bleach — iwa ili iwe nyeupe. Kupikwa kwa joto la hali ya juu sana. Kunaifanya isifae kiafya. Madini ya ‘iodine’ yanayopatikana katika chumvi asili hayatoshi kuzuia ugonjwa wa rovu. Ndio maana huongezewa ‘potassium-iodide’ ili kukukinga na ugonjwa huo. Ikumbukwe kwamba madini yanayoongezwa kwenye chumvi asili sio asili. Bali yametengenezwa kiwandani na hivyo moja kwa moja. Haya hayafai kuingia mwilini mwako. Badala yake tumia chumvi asili ya mawe. Na kula vyakula vyenye madini ya ‘iodine’ kwa wingi. Kama vile maziwa na mayai.

Pombe

Matumizi yaliyokithiri ya pombe yanaweza kusababisha matatizo ya ini, ugonjwa wa moyo.Na saratani. Pia pombe huweza kusababisha unene aka ‘beer belly’ kwa mtumiaji aliyekithiri. Matatizo ya pombe ni mengi, mengi sana. Ulevi kupindukia ni tishio kwa uchumi wa mtumiaji.
Hivyo ni baadhi tu ya vyakula ambavyo hupaswi kuvila. Kutokana na madhara yanayoletwa na vyakula hivyo kiafya. Ni vema binafsi kila mtu akajihoji anajisikiaje baada ya kutumia chakula fulani. Huenda chakula fulani kikawa kibaya kwa mtu huyu. Lakini kikawa bora kwa mtu mwingine. Pia ni vema kila mtu akawa muwazi kwa tafiti mbali mbali zinazokuwa zimefanywa na wataalamu wa afya.
Share: