Tuesday, July 7, 2020
Home »
» HEDHI KIPINDI CHA UJAUZITO
HEDHI KIPINDI CHA UJAUZITO
| Katika hali ya kawaida,hedhi ya mwanamke hufikia ukomo pale tu anapopata ujauzito. Kwa baadhi ya wanawake,siku chache hata baada ya kugundua kuwa ni wajawazito hutokwa na damu ambayo mara nyingi huwa na rangi nyeusi au hata dark brown. Hii siyo hedhi Kuna sababu kadhaa ambazo husababisha kutokea kwa hali hii. Miongoni mwa sababu hizo ni kujishikiza kwa kijusi kwenye mji wa uzazi,ambapo huchimba ukuta wake na kusababisha kutokwa na damu hii. Hili ni jambo la kawaida kabisa,siyo tatizo na hutokea walau siku 10-14 tangu siku ya kutungwa kwa ujauzito
- Sababu zingine ni kuwa na ujauzito nje ya mji wa uzazi (Ectopic pregnancy),mabadiliko kwenye shingo ya kizazi,maambukizi pamoja na tishio la kuharibika kwa ujauzito husika. Mara nyingi hali hii huambatana na maumivu makali ya nyonga na mgongo maumivu ya mabega,uchovu mkubwa bila sababu,kukata kwa pumzi na kupitia mabadiliko makubwa kwenye aina ya ute unaotolewa kwenye sehemu za siri Hali hizi zote ni dharura na mwanamke anapaswa kufika hospitalini siku hiyohiyo kabla jua halijazama.