Monday, July 6, 2020

UZITO KUPITA KIASI / OVER WEIGHT (OBESITY)

UTAFITI: KITAMBI KINAONGEZA HATARI YA KUPATA SARATANI - Mtanzania KUPITA KIASI / OVER WEIGHT (OBESITY)


UZITO KUPITA KIASI (OVER WEIGHT) ni uzito was mwili ambao umezidi au nimkubwa kuliko unaostahili kiafya kutokana na urefu alionao mtu.
SABABU ZA UZITO MKUBWA
Mafuta mengi mwilini kuliko yanayohitajika kiafya husababisha uzito kuwa mkubwa, sababu zingine ni kama mazingira,umri mkubwa,vyakula kiasi kingi na aina ya chakula mtu anachopendelea hasa vyenye wanga au sukari,historia ya familia,genetics, nguvu inayoingia mwilini ikiwa kubwa kuliko inayoingia,matatizo ya kiafya hasa matatizo ya homoni,kukosa usingizi,ujauzito na kutokufanya mazoezi
VITU VITAKAVO KUSAIDIA KUPUNGUZA UZITO
~Kula chakula cha kutosha lakini hakikisha unapunguza au unaepuka kula chakula cha aina ya wanga au sukari,mlo wako use na vyakula vya protein, Mafua na mboga za majani kwa wingi.kwa mfano kula mayai,mboga za majani,nyama,samaki,Nazi(juisi au upikie) na olive oil.
~Fanya mazoezi ya viungo vya mwili mara kwa mara kama kutembea,kukimbia n.k hii itasaidia calories nyingi kutumika.
~Hakikisha hormone zako ziko vizuri kwa kula vyakula vyenye kiasi kidogo cha carbohydrate,kutumia Dawa asili zinazo weka homoni sawa na upendelee kupima iliujue ziko vipi.maana homoni zikiwa haziko vizuri utapata matatizo kama utendaji kazi wa mwili hautakuwa mzuri hivyo calories hazitatumika kiasi kikubwa hivyo kuongezeka uzito,pia utaona unapata matatizo mengine kama misuri kukaza,choo ngumu,ngozi kuwa kavu,na kuhisi baridi kari.
~Epuka vilevi hasa bia kwani ina carbohydrate ambayo ni chanzo cha kuongeza uzito uliozidi kama hauwezi kuacha basi ni bora kutumia wine na pure spirit.
~Kula ukiwa unahisi njaa tu sio lazima ule kwa mazoea.
~Epuka mambo yanayokufanya uwe na msongo wa mawazo, pia unatakiwa ulale Masaa ya kutosha angalau 7-8 kwa siku.
~Pendelea kula vyakula asilia tu vyenye kukupatia madini na vitamini za kutosha hivyo epuka vyakula vya viwandani.
Share: