Saturday, June 13, 2020

UGONJWA WA MATENDE(elephantiasis)

UGONJWA WA MATENDE(elephantiasis)
๐Ÿ’ซUgonjwa wa matende ni aina ya ugonjwa unaosababisha ngozi na tishu zilizo chini ya ngozi ya mwanadamu kuwa nene (thickening of skin and underlying tissue).Ugonjwa huu huathiri miguu, mikono, figo, korodani na kusababisha korodani kuvimba na kuwa kubwa sana.Inakisiwa watu milioni 120 duniani wanao ugonjwa uu, theluthi moja wapo Africa...
๐Ÿ’ซUgonjwa wa matende husababishwa na vimelea aina ya minyoo (parasitic worm) vinajulikana kama Wuchereria bancrofti, Brugia malayi, B. timori ambavyo huenezwa na mbu jike aina ya culex quinquefasciatus mosquitoes na jamii fulani ya mbu dume (Anopheles species) wakati minyoo aina ya Brugia roundworms huenezwa mbu wanaojulikana kama Mansonia mosquitoes. Mbu hawa hueneza ugonjwa huu kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwengine.
๐Ÿ’ซAina nyingine ya ugonjwa wa matende inayojulikana kama nonparasitic elephantiasis au podoconiosis ambayo haisababishwi na vimelea vyovyote hupatikana katika nchi za Afrika Mashariki (Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda, Burundi) Sudan,Egypt...
๐Ÿ’ซNini hutokea baada ya maambukizi?
Kwa kawaida mtu aliyeambukizwa ugonjwa huu huwa na mabuu (larvae) kwenye mfumo wa damu mwilini mwake wanaojulikana kama microfilariae. Mabuu haya husafiri kutoka kwenye mfumo wa damu hadi kwenye mfumo mwingine unaojulikana kama mfumo wa limfu (lymphatic system) na kukua kuwa minyoo kamili (adult worms) ambayo huziba mfumo huu wa limfu ambao unategemewa sana katika kuweka uwiano sawa wa maji (fluid balance) kati ya mfumo wa damu na tishu ndani ya mwili na husaidia kuupa mwili kinga dhidhi ya magonjwa mbalimbali
๐Ÿ’ซMinyoo hii huishi kwa miaka minne hadi sita na katika uhai wake huzaa mamilioni ya mabuu (microfilariae) mengine wakati ikiwa kwenye mfumo wa damu.
๐Ÿ’ซMbu huenezaje ugonjwa huu?
Mtu ambaye ameambukizwa ugonjwa huu huwa na mabuu kwenye mfumo wake wa damu na anapongatwa na mbu ambao wanauwezo wa kuchukua mabuu haya ambayo huendelea kukua na kufikia hatua ya kuambukiza mtu mwingine ndani ya mwili wa mbu.Kwa kawaida, ukuaji huu wa mabuu ndani ya mwili wa mbu huchukua wiki moja hadi tatu na baada ya kukua na kufikia hatua ya kuambukiza mtu mwingine, mabuu haya husogea mpaka kwenye sehemu ya mdomo wa mbu ambayo ndio huwa humng'ata mtu wakati mbu anapofyonza damu kutoka kwa mtu. Mbu mweye mabuu kwenye mdomo wake anapomngata mtu ili kufyonza damu, ndipo mabuu haya yanapoingia kwenye mwili wa mtu na hivyo kusababisha maambukizi ya ugonjwa huu.
๐Ÿ’ซDalili za ugonjwa huu ni zipi?
โ€ขKuvimba sehemu ya chini ya mwili yaani kwenye miguu na vidole.Pia mtu anaweza kuvimba sehemu ya mikono au mkono wote pamoja na vidole vya mkononi. Wengine huvimba kwenye korodani (wanaume).
โ€ข Kuhisi uzito na kukamaa kwa mikono au miguu kutokana na uvimbe uliopo.
โ€ข Kutoweza kutumia kiungo husika kilichovimba.
โ€ข Maumivu au kutohisi vizuri kwenye mikono au miguu.
โ€ข Kupata maambukizi ya mara kwa mara kwenye sehemu iliyovimba.
โ€ข Ngozi kuwa nene na ngumu kwenye mikono au miguu.
Dalili nyingine ni pamoja na
Homa
Maumivu ya kichwa
Maumivu kwenye jointi na mifupa
Kutapika
Vidonda kwenye mikono au miguu
Mistari ya rangi nyekundu inayoonekana kwenye mikono au miguu ..
๐Ÿ’ซTiba ya ugonjwa wa matende ni nini?
Tiba ya ugonjwa wa matende hutegemea na sehemu husika.

๐Ÿ’ซKinga ya ugonjwa wa matende ni nini?
โ€ข Shirika la afya duniani (WHO) limeanzisha jitihada za kutokomeza ugonjwa huu wa matende ifikapo mwaka 2020.
โ€ข Kuvaa viatu wakati wa kutembea nje ili kujikinga kupata maambukizi ya aina ya podoconiosis.
โ€ข Kuosha miguu na mikono kwa kutumia maji na sabuni
โ€ข Kuosha miguu kila siku kwa kutumia antiseptic (bleach).


Share:

Related Posts: