Monday, June 22, 2020

MADHARA YA KULA NYAMA MBICHI

MAPISHI YA NYAMA

Nyama ni chakula ambacho kimekuwa kikiliwa tangu enzi za mababu zetu. Pamoja na kuwa chakula chenye virutubisho kwa afya ya mwanadamu, pia kumekuwa na mgongano wa mawazo juu ya ulaji wa nyama mbichi, hususani faida au harasa zozote zinazopatikana kwa mtu kula nyama mbichi.
Kwa baadhi ya jamii swala la kula nyama mbichi ni kitu cha kawaida, na hasa jamii za wafugaji, na kuna baadhi ya watu wanakula nyama mbichi bila ya wao kuelewa, hii ni katika vyakula vinavyoandaliwa katika maeneo mbalimbali ya kutolea huduma za chakula, mfano wachoma mishikaki au vyakula vinavyofahamika sana kwa jina la TakeAway or Fast-Food.
Kabla hatujaenda mbali katika kuzungumzia nyama mbichi, tuangalie ni vitu gani muhimu vinavyopatikana katika nyama:
Nyama huwa na vitamini (Vitamin B3, Vitamin B6, Vitamin B12), madini ya chuma (Iron), Zinc, Selenium, pia katika nyama kuna mafuta (Fat), protini ambayo hufanya kazi ya kuujenga mwili na pia kuna madini mengine na virutubisho vingi ambavyo huujenga mwili na kuuweka katika hali ya afya zaidi.
Pamoja na kuwa na virutubisho hivyo, bado ukweli unabaki kuwa, nyama hutofautiana kwa kuwa haziandaliwi au kutengenezwa katika mazingira yaliyo sawa. Nyama itokanayo na mnyama anayekula majani porini (wanyama pori), nyama ya wanyama wa kufugwa na kadhalika, zote hizi hutofautiana, na pia utaalamu unaotumika katika kuiandaa nyama mpaka wewe mlaji inakufikia na kuanza kuila, pia unatofautiana. Vitu vyote hivi kwa pamoja huchangia nyama iwe na usalama kiasi gani kwa mlaji.
Mara nyingi wanyama wa kufugwa, ng’ombe, kuku au nguruwe, huwa wanalishwa vyakula na madawa au kemikali ambazo mfugaji anakuwa anahitaji mifugo yake ikue haraka na kama ni biashara basi, apate faida mapema. Wewe na mimi kama walaji wa nyama, hatujui huyo kuku au ng’ombe alilishwa nini, nyama yake tunapoitumia ikiwa mbichi mfano katika mishikaki isiyoiva vizuri (watu wengi hupendelea kula mishikaki, bila ya kujali ni ya chelewa au la..) kiafya madhara yanayoweza kumpata mtu ni pamoja na, hatari ya kupata magonjwa ya tumbo yasababishwayo na wadudu jamii ya Salmonella (kuharisha damu, kutapika, maumivu ya kichwa na homa), nyama mbichi (red meat) huwa na damu damu ambazo kiafya huongeza hatari ya mtu kupata magonjwa ya moyo.
Nyama iliyotokana wa wanyama wanaokula vitu asilia, mfano wanyama pori, kwa kiasi kikubwa haina hatari ya kuwa na kemikali au vitu hatarishi kama ambavyo vinapatikana kwa wanyama wengine wanaolishwa madawa na kemikali za kuwafanya wakue haraka.
Kama wewe ni mpenzi wa kula nyama, ni vyema ukawa makini na aina ya nyama unayokula, je imeandaliwa vipi?. Kula nyama iliyoiva au kupikwa vizuri ili uepukane na magonjwa mbalimbali yatokanayo na ulaji wa nyama iliyoandaliwa vibaya au mbichi.
Share: