VITAMINI C
Ni vitamin muhimu ambayo hupatikana kwa kula maana mwili hauitengenezi. Na haikai mwilini hutumika wakati huo huo.
Ni vitamin muhimu ambayo hupatikana kwa kula maana mwili hauitengenezi. Na haikai mwilini hutumika wakati huo huo.
Kwanini inahitajika mwilini?
Kwa ajili ya ukuaji na urekebishwaji wa tishu katika sehemu mbalimbali za mwili. Inasaidia mwili kujenga Collagen - protini muhimu inayojenga ngozi, makole ya kwenye viungo(cartilage), nyuzinyuzi(tendons), na mishipa ya damu(arteries). Pia Collagen ni tishu inayosaidia kizishikilia seli pamoja.
Ni muhimu kwa afya na kuimarisha mifupa, meno, fizi na mishipa ya damu. Inasaidia mwili kufyonza madini ya chuma, inasaidia kuponya vidonda na kazi za ubongo.
Inafanyaje kazi
Vitamin C pia ikijulikana kama asidi ya Ascobic, ni kirutubisho kinachopenya kwenye maji na hupatikana kwenye vyakula. Katika mwili kinafanya kazi kama kiosha sumu, husaidia kulinda seli zisiharibike na Free radicals. Free radicals ni kompoundi zinazojengwa na mwili wakati unabadilisha chakula tunachokula kwenda kwenye Nguvu au wakati mwili umeingiliwa na sumu kutoka kwenye vyakula, mazingira, viifadhio vya vyakula na rangi za kutengenezwa za vyakula
Kwa Ngozi
Vitamin C inavyofanya ni kuondoa ngozi iliyochoka na kusaidia ngozi yako kuwa mpya. Majaribio yanaonyesha unaweza kurudisha miaka ya ngozi yako na kionekana ipo miaka 10 au 20 nyuma kwa kitumia vitamin C.
Kwa seli za Saratani
Vitamin C ni kiosha sumu kikubwa kinacho jenga white blood cells ambao ni mfumo wa kinga ya mwili juu ya madhara yaFree radicals.
Pia utafiti unaonyesha vyakula vyenye Vitamin C vinaweza kupunguza uwezekano wa kupata Saratani, zaidi saratani ya mdomo,Kongosho,Tezi Dume, Ini na mmeng'enyo wa chakula haya yameelezwa na Jane Higdon, mwana sayansi ya lishe huko Linus Pauling Institute- Oregon State University. Vitamin C ni kiosha sumu muhimu kinacho ondoa molecules za oxygen ambazo haziko sawa au hazijakamilika. Ambazo zingeharibu DNA. Pia utafiti wa karibuni umeonyesha pia inasaidia kuzuia bakteria aitwaye Helicobacter Pylori anaye sababisha vidonda vya tumbo na kansa ya utumbo. Utafiti wa 2003 Huko San Francisco Veterans Affairs Medical Center walirepoti kwamba watu wenye Vitamin C nyingi kwenye damu yao sio rahisi kuathiriwa na bacteria H. pylori. Vitamini C zinazuia ukuaji wa bacteria.
Kwa Moyo
Vitamini C pia ni rafiki wa arteries na moyo. Utafiti ulifanywa kwa wanawake 85,000 huko Boston katika hospitali ya watoto mwaka 2003 na kugundua wale walio tumia vitamin C nyingi hawakuwa na athari ya magonjwa ya moyo kwa kipindi chote cha miaka 16. Hapa pia usafishaji wa sumu utakuwa umesaidia kuziacha arteries kuwa safi na kutokuwa na cholesterol.

Kwa wajawazito
Hudaidia kuimarisha kinga na ufyonzwaji wa madini ya Chuma yanayosaidia kujenga damu na pia kukufanya usisikie kichefuchefu.
Utumiaji wa vitamin C ya kutosha kwa mama na na mtoto. 2014 huko Seoul,South Korea walireport watoto wenye uzito mkubwa walizaliwa na wamama waliotumia vitamin C ya kutosha. Mwaka huu utafiti katika European Journal of Clinical Nutrition walishauri utumiaji wa vitamin C wakati wa kunyonyesha walipunguza matatizo ya Dermatitis kwa watoto.
Vitamin C ni muhimu katika kulinda na kujenga Connective Tissue.
Ukosefu wa vitamin C
Unaleta uvimbaji na utokaji damu wa fizi, ngozi kupauka, kutoka damu puani, maumivu kwenye viungio vya mwili na maradhi mengine yanayo oanishwa na SCURVY.
Unaleta uvimbaji na utokaji damu wa fizi, ngozi kupauka, kutoka damu puani, maumivu kwenye viungio vya mwili na maradhi mengine yanayo oanishwa na SCURVY.
Je unahitaji kiasi gani?
Wanaume wanashauriwa kutumia 90mg na wanawake 75mg kila baada ya masaa 4.
Wanaume wanashauriwa kutumia 90mg na wanawake 75mg kila baada ya masaa 4.
Wanasayansi wameripoti kwamba matumizi ya sigara moja yanaondoa 25mg ya Vitamin C. Msongo wa mawazo, matumizi ya madawa na uchafuzi wa mazingira hupunguza sana vitamini C katika mwili.
Utafiti ulifanyika pia Machungwa yalichumwa mtini na chungwa la juu lilikuwa lina 120mg za vitamin C baada ya kuanza kusafirishwa na kuhifadhiwa likapungu baadhi yakapungua mpaka 60mg na machungwa mengine yalipoteza kabisa vitamin C.
Ingawa tuna kula vyakula vizuri kama matunda na vyakula vyenye vitamin C bado miili yetu inakosa Vitamin C kwa sababu ya mazingira, usafirishaji, udongo uliochoka, mbolea za kemikali na vyakula vya haraka.
Pia vitamin C hupotea haraka mwilini kwasababu ni water soluble wakati inahitajika sana.