Tangu enzi na enzi zao la Asali (mathalani asali mbichi), limekuwa likitumika kutibu magonjwa mbalimbali kwa ufanisi mkubwa huku vitabu vingi vikiandika ni kwa namna gani watu wengi wameweza kutibiwa na mchanganyiko wa Asali na Mdalasini.
Licha ya kuaminika kutumika katika huduma ya kwanza pale mtu anapokuwa ameungua, ASALI imekuwa dawa yenye nguvu na ubora wa hali ya juu hasa pale inapochanganywa na dawa zingine (mitishamba) kama vile MDALASINI ikiwemo kutibu kwa asilimia zote tatizo lupungufu wa nguvu za kiume.
Muunganiko wa Asali na Mdalasini unaimarisha afya ya mwili kwa ujumla, na wengi wanakiri maajabu yaliyomo katika mchanganganyiko wa ASALI na MDALASINI.
Kwa mujibu wa wataalam, mdalasini na asali kwa pamoja hutengeneza uwiano sahihi wa joto na baridi mwilini na kwa pamoja kutengeneza muunganiko mmoja muhimu wa dawa dhidi ya maambukizi ya mgonjwa mwilini kama yafuatayo;
- Ugonjwa wa Moyo: Utumiaji wa mchanganyiko wa asali na mdalasini mara kwa mara mwilini husaidia kuepuka ugonjwa wa moyo na kuepusha kuzibika kwa mishipa ya ateri katika moyo wa binadamu ambayo ni muhimu kwa usafirishaji wa damu. Pamoja na mchanganyiko wa asali na mdalasini, ufanyaji wa mazoezi ya viungo mara kwa mara, ulaji wa chakula bora, na kuepuka kukaa kwenye kiti kwa masaa mengi ni muhimu kwa afya ya moyo wa binadamu.
- Inatibu maambukizi katika kibofu cha mkojo: Asali na Mdalasini kwa pamoja ni dawa bora kwa watu wenye maambukizi katika kibofu cha mkojo dhidi ya wadudu (bacteria) wanaoshambulia kibofu cha mkojo. Mchanganyiko huo husafisha kibofu na kukiweka kuwa katika hali ya usafi wakati wote na hivyo kuepusha maambukizi katika eneo hilo la mwili.
- Hutibu Fizi kutoa damu: Kama una tatizo la fizi kutoa damu bila sababu yoyote, mchanganyiko wa asali na mdalasini ni suluhisho bora kwa tatizo hilo. Asali mbichi na mdalasini husaidia tatizo la fizi kutokwa damu, kuuma kwa fizi, ganzi katika meno na maambukizi mengine katika fizi. Unaweza kupaka mchanganyiko huo katika mswaki na kutumia kama mbadala wa dawa ya meno na kusafisha meno yako kwa faida zaidi ya afya ya meno na fizi zako.
- Kutibu meno yaliyotoboka: Mbali na kutibu vyema matatizo ya fizi, mchanganyiko wa asali na mdalasini unaaminika kusaidia vyema tatizo la kutoboka kwa meno. Mchanganyiko huo huua vijidudu (bacteria) mbalimbali wasababishao meno kutoboka. Tumia mchanganyiko huo kama ya meno asubuhi unapoamka na jioni kabla ya kulala.
- Husaidia katika mfumo wa mmeng’enyo wa chakula: Asali na mdalasini kwa pamoja husaidia kusafisha utumbo mpana kwa kuondoa sumu na taka zote na kusaidia uzalishwaji wa bacteria maaluum kwa ajili ya umeng’enyaji wa chakula.
- Huondoa Gesi Tumboni: Asali yenye mdalasini husaidia sana kulinda tumbo kwa kufunika kuta za tumbo na hivyo kusafisha mfumo wa bacteria wabaya, kutibu maambukizi yoyote na kusaidia vyema kutibu tatizo la tumbo kujaa gesi au acid (asidi).
- Huongeza akili: Wataalam wanazidi kusema kuwa asali yenye mdalasini ina uwezo mkubwa wa kuimarisha ubongo na kuweza kufanya kazi yake ipasavyo pamoja na kuimarisha kumbukumbu katika akili ya mwanadamu.
- Kusaidia kutibu Kansa: Ingawa bado haijathibitishwa kwa asilimia 100 ni jinsi gani mchanganyiko wa asali na mdalasini unavyoweza kutibu tatizo la kansa, mchanganyiko huo unaaminika kuwa na uwezo wa kuondoa sumu na vimelea vingine vya magonjwa (free radicals) na kuwa msaada mkubwa katika utibuji wa kansa.
- Inaongeza Nguvu ya mwili: Mchanganyiko wa asali na mdalasini una madini kadhaa muhimu kwa mwili wa binadamu kama vile chuma, vitamin C, vitamin K, calcium, na fiber (nyuzinyuzi) ambapo kwa pamoja huongeza kinga katika mwili na kuupa nguvu zaidi hasa kwa akina baba katika nguvu ya kufanya tendo la ndoa.
- Hutibu Chunusi: Mchanganyiko wa asali na mdalasini husaidia sana kutibu magonjwa mbalimbali ya ngozi ikiwemo kutibu chunisi na mba. Asali hudhibiti bacteria wakati mdalasini hudhibiti maambukizi na kuondoa sumu katika ngozi. Mchanganyiko huu unapaswa kupakwa katika ngozi kama mafuta na kuachwa kubaki juu ya ngozi kwa muda mrefu.
- Husaidia kuotesha nywele: Mchanganyiko wa kijiko kidogo cha asali, mafuta ya mzeituni, na kijiko cha chai cha mdalasini husaidia uotaji wa nywele mwilini.
- Kutibu harufu mbaya mdomoni: Mcanganyiko wa asali na mdalasini unasifika kwa kutibu tatizo la harufu mbaya mdomoni kwa kutumia mchanganyiko huo wa kijikokimoja cha chakula kwa kuchanganya na maji ya uvuguvugu kila pale muathirika wa tatizo hilo anapoamka asubuhi. Mchanganyiko huo utakufanya kuwa na harufu nzuri na kupumua vyema kwa siku nzima.
- Hutibu Ugumba: Asali na mdalasini inaaminika katika kusaidia tatizo la ugumba linalowatesa watu wa jinsia zote. Inashauriwa kutumia mchanganyiko huo kwa kula vijiko viwili vya chakula kila unapoamka asubuhi kabla ya kula kitu chochote na pale unapoenda kulala.
- KUSAIDIA KWA UKAMILIFU TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME: Kazi kubwa ya mchanganyiko wa asali mbichi na mdalasini ni kutibu tatizo la upungufu wa nguvu za kiume kwa asilimia 100. Tumia mchanganyiko huo kwa kuweka vijko vitatu vya chakula katika maji ya moto, kisha acha mchanganyiko huo utulie kwa dakika 15 kisha kunywa. Tumia glasi moja asubuhi kabla ya kula kitu chochote na glasi moja kabla ya kwenda kulala, utaona mabadiliko katika ndoa yako.
Zifuatazo ni mbinu za kuitambua asali ambayo ni salama kwa maana ya kwamba haijachakachuliwa:
• Weka maji kwenye glasi na kisha mimina asali ndani yake na kwamba ikikaa chini ya glasi bila kuchanganyana na maji basi hiyo ni asali asilia na inakuwa haijachanganywa na chochote.
• Njia ya pili ni kuiweka asali kwenye njiti ya kibiriti na kisha kuiwasha hiyo njiti ya kiberiti, ikiwa njiti hiyo itawaka basi asali haijachakachuliwa kwa kuchanganywa na chochote lakini njiti ya kiberiti isipowaka asali hiyo inakuwa ni feki.
• Njia nyingine ni kuionja bidhaa hiyo na kwamba iliyochakachuliwa kwa kuchemshwa hutoa harufu ya moshi tofauti na ambayo ni halisi (original).