Thursday, June 18, 2020

FAHAMU UGONJWA WA PUMU NA TIBA YAKE

FAHAMU UGONJWA WA PUMU NA TIBA YAKE
Asalaam alaykum warhmatullah wabarakatul, ni matumaini yangu wote tuwazima alhamdulillah kwa nafasi ya kukutana tena hapa kupata somo la afya kuhusu ugonjwa wa pumu ambao umekuwa ukiwatesa watu sana
Naam
Ugonjwa wa pumu ni ugonjwa ambao huathiri sehemu ya kupitisha hewa kwenda kwenye mapafu ya binadamu zinazojulikana kitaalamu kama bronchioles. Mtu mwenye pumu huwa na mcharuko mwili sugu (chronic Inflammation) kwenye mirija yake ya
kupitishia hewa (bronchioles tubes)hali ambayo husababisha kuvimba kwa kuta za mirija hii, kujaa kwa ute mzito (mucus) na kupungua kwa njia ya kupitishia hewa, hali ambayo humfanya muathirika kushindwa kuvuta na kutoa hewa
nje na hivyo kupumua kwa shida sana. Hali hii inaweza kudumu kwa muda mfupi au mrefu kiasi cha kuhitaji tiba ili kumuwezesha mgonjwa kupata nafuu. Kutokana na kuwepo kwa msuguano na uzuiaji wa kupitisha hewa wakati wa kupumua hwa nje, pumu hujulikana pia kama obstructive lung disease . Mtu aliye na pumu, huwa nayo kipindi chote cha maisha yake.
MAKUNDI YA PUMU
Pumu inaweza kugawanywa katika makundi mawili;
Pumu ya ghafla (Acute asthma): Wagonjwa wanaopatwa na kundi hili la pumu huwa na hali ya kawaida katika njia zao za hewa isiyobadilika kati ya shambulizi moja na jingine.Pumu sugu (Chronic Asthma): Kundi hili la pumu huwa na tabia ya kuwa na njia nyembamba za kupitisha hewa na kadiri jinsi mgonjwa anavyoendelea kupata matukio zaidi ya pumu, njia za hewa huzidi kuwa nyembamba zaidi.
AINA ZA UGONJWA WA PUMU
Bila kujalisha mgonjwa anaingia katika kundi gani, ugonjwa wa pumu unaweza kugawanywa katika aina kuu nne, ambazo ni 1.Pumu inayobadilika (brittle asthma):Kulingana na tabia ya kujirudia rudia kwa matukio ta ugonjwa huu na madhara yake kwa mgonjwa, aina hii ya pumu inaweza kugawanywa zaidi katika aina nyingine mbili, ambazo ni
Aina ya kwanza ya pumu inayobadilika (type 1 brittle asthma) ni pumu yenye tabia ya kuwa na matukio na mashambulizi ya kubadilika kila mara japokuwa mgonjwa anaweza kuwa anapata matibabu kadhaa.Aina ya pili ya pumu inayobadilika (type 2 brittle asthma) ni pumu ambayo mgonjwa anatokea kupata shambulizi la ghafla(asthmatic attack) wakati hapo awali ugonjwa wake uliweza kuthibitiwa kwa matibabu.2.Pumu hatari isiyobadilika (status asthmaticus): Hii ni aina ya pumu iliyo hatari zaidi kwa mgonjwa. Pamoja na
matumizi ya dawa kadhaa,zikiwemo vitanua njia za hewa(bronchodilators) na vipoza mcharuko mwili (steroids), mgonjwa wa aina hii ya pumu anaweza asipate nafuu ya haraka, na anaweza kupoteza maisha. 3.Pumu
inayosababishwa na mazoezi(Exercise Induced Asthma): Hali hii husababishwa na ufanyaji wa kupitiliza wa mazoezi ya viungo. Kwa kawaida wakati wa kufanya mazoezi mtu hupumua kwa kutumia pua na kupitia mdomoni. Hata hivyo wakati
mwingine hutokea hewa aivutayo huingia ndani ikiwa haijapozwa vya kutosha puani na hivyo kusababisha ongezeko la mtiririko wa damu katika mishipa inayosambaza damu katika mirija ya kupitisha hewa. Hali hii husababisha kuvimba
kwa kuta za mirija hiyo na muhusika kupata shambulizi la pumu. Aina hii ya pumu yaweza kudhibitiwa na dawa. Inashauriwa sana kwa watu wenye matatizo kama haya kupasha moto misuli kwa mazoezi mepesi (warming up)kabla
ya kuanza mazoezi mazito na ya muda mrefu. 4.Pumu inayosababishwa na aina ya kazi afanyayo muhusika (Occupational Induced Asthma): Wakati fulani, mazingira ya kazi yanaweza kusababisha kutokea kwa pumu hata kwa baadhi ya wafanyakazi wasio na tatizo hili. Mara nyingi aina hii huweza kuwatokea watu wanaofanya kazi kwenye viwanda vya kutengeneza matairi, vigae, rangi, kemikali mbalimbali, mbolea, chuma, unga na mbao.
VISABABISHI VYA PUMU
Kuna mambo kadhaa yanayoweza kusababisha kutokea kwa pumu au yanayohusishwa na shambulizi lake. Mambo hayo ni pamoja na
Matatizo ya kinasaba: Matatizo ya kinasaba yamehusishwa na kutokea kwa karibu asilimia 90 ya ugonjwa wa pumu hususani kipindi cha utoto.Uvutaji wa sigara au tumbaku kipindi cha ujauzito pia unahusishwa na kusababisha pumu kwa mtoto atakayezaliwa.Maendeleo ya kiuchumi: Ugonjwa wa pumu umeonekana sana kwenye nchi zilizoendelea kiuchumi ikilinganishwa na nchi zenye maendeleo na hali duni ya kiuchumi.Magonjwa ya mapafu kamabronchitisVyanzo vya mzio(allergens)kama vile vumbi, vinyesi vya wanyama na baadhi ya vyakula.Uchafuzi wa mazingira kama moshi na baadhi ya harufu kali.Baadhi ya kemikali kwenye maeneo ya kazi hasa kwenye viwanda kama vya rangi, chuma, sementi na vigae.Baadhi ya wagonjwa wanaotumia dawa za kushusha shinikizo la damu zilizo katika jamii ya beta-blockers kama vile propanololwapo katika hatari ya kupata shambulio la ugonjwa wa pumu.Magonjwa kwenye mfumo wa kupumua yasabishwayo na baadhi ya virusi na bakteria kama vile rhinovirus, Chlamydia pneumonia auBordetella pertusis.Matumizi ya mapema sana ya baadhi ya dawa hasa antibiotiki kwa watoto yanaweza kubadilisha mfumo wa kinga ya mwili dhidi ya magonjwa na hivyo kumfanya mtoto kuwa katika hatari ya kupata pumu.Ongezeko la msongo wa mawazo huweza kusababisha pumu na matatizo katika mfumo wa upumuajiUpasuaji wakati wa kujifungua (caesarian section):Tafiti kadhaa zimeonesha kuwa kujifungua kwa njia ya upasuaji huongeza uwezekano wa kupata pumu kwa vile njia hiyo yaweza kuathiri mfumo wa kinga ya mwili dhidi ya maradhi.Vihatarishi vya ugonjwa wa pumu
Uwezekano wa kupata ugonjwa wa pumu huongezeka iwapo mtu
Atakuwa na magonjwa ya mzio kama vile magonjwa ya ngozi (eczema) au homa isababishwayo na aina fulani ya vumbi (hay fever)Atavuta chavu (pollen) kutoka kwenye maua au mitiAtajihusisha na uvutaji sigaraAna historia ya ugonjwa wa pumu au mzio kwenye familiaUtumiaji wa dawa aina yaaspirinAna msongo wa mawazoAna uambukizi wa magonjwa ya virusi kamarhinovirusMazoeziAnaishi sehemu zenye baridiAna matatizo katika njia yake ya chakula (Gastroesophageal reflux disease au GERD)
DALILI ZA PUMU
Dalili za ugonjwa wa pumu ni pamoja na
Kuishiwa na pumzi na kupumua kwa shida (shortness of breath)Kutoa sauti kama mtu anayepiga miluzi wakati wa kupumua (wheezing)Kukohoa sana (chronic cough)hasa nyakati za usiku au asubuhi. Aidha kikohozi huambatana na kutoa makohozi mazito, yasiyo na rangi au yenye rangi ya njano.Kubana kwa kifua.Kwa mtu aliyepata shambulizi kubwa la pumu (severe asthmatic attack) anaweza kushindwa kuzungumza na pia kuwa na hali kama ya kuchanganyikiwa.Vipimo na Uchunguzi
Pamoja na daktari kutaka kufahamu historia ya mgonjwa, anaweza pia kuamua kufanya vipimo vifuatavyo ambavyo vitamsaidia kufahamu chanzo na madhara ya ugonjwa wa pumu kwa muathirika.
Kipimo cha damu (complete blood count) msisitizo ukiwa kwenye wingi wa seli za damu aina ya eosinophils ambazo uhusika na kuwepo kwa shambulio la mzio.Kipimo cha kuchunguza uwezo wa mgonjwa kutoa hewa nje mara baada ya kuivuta (spirometery). Aina hii ya uchunguzi hufanyika kabla ya mgonjwa kupewa dawa kwa kutumia nebulizer.Kipimo cha kuchunguza kiwango cha hewa ya oksijeni kilichopo kwenye damu ya mgonjwa (oximetry).Kipimo cha kuchunguza uwezo wa mgonjwa kupumua hewa nje wakati wa shambulizi la pumu (Peak flow meter).X-ray ya kifua kwa ajili ya kutofautisha pumu na magonjwa mengine yenye dalili za kufanana kama vile ugonjwa wa moyo (congestive heart failure), magonjwa sugu ya kuziba kwa njia za hewa (COPD kama vile chronic bronchitis na emphysema) na magonjwa mengine ya kuzaliwa kama vile cystic fibrosis.Kipimo cha mzio cha ngozi(skin allergy test) kwa ajili ya kutambua aina ya mzio inayomsababishia mgonjwa shambulizi la pumu.
MATIBABU YA PUMU
Kwa ujumla matibabu ya pumu hujumuisha kuepuka visababishi vya ugonjwa huu na matumizi ya madawa kwa walio na hali mbaya. Aidha, kwa wanaopata ugonjwa huu kwa sababu ya msongo wa mawazo hupewa ushauri nasaha kwa ajili ya
kusaidia kutatua matatizo yanayowakabili. Vilevile inashauriwa kwa wenye tatizo hili, kuwa na dawa karibu muda wote kwa ajili ya matumizi pindi shambulizi litakapotokea. Pia inashauriwa sana kuepuka mazingira na hali za baridi ambazo
huweza kuchochea kutokea kwa shambulio la ugonjwa huu. Matibabu ya kutumia dawa hujumuisha matumizi ya dawa za kusaidia kupunguza na kuondoa makohozi (expectorants), dawa zinazosaidia kutanua mirija ya hewa(bronchodilators), dawa za kuondoa mcharuko mwili kama vile cortisone ya drip (hasa wakati wa dharura) au nebulizer, na dawa za kuzuia
mzio (antihistamine drugs). Hata hivyo, kuna matibabu ya ziada kulingana na hali ya mgonjwa pamoja na kundi na aina ya pumu inayomuathiri mgonjwa. Kwa wagonjwa wenye pumu ya ghafla na wenye hali mbaya (acute asthma)matibabu hujumuisha matumizi ya dawa za kutanua mirija ya hewa(bronchodilators) pamoja na kuongezewa hewa ya
oksijeni, dawa za kutuliza mcharuko mwili (steroids) pamoja na dawa za kutuliza kukakamaa kwa misuli ya mwili (intravenous muscle relaxants). Aidha kwa vile mara nyingi shambulizi hili laweza kuwa la hatari sana, mgonjwa hulazwa
hospitali na huongezewa hewa ya oksijeni, na kwa wagonjwa wasioweza kupumua kabisa, husaidiwa kufanya hivyo kwa kutumia mashine maalum iitwayo(mechanical ventilator). Kwa wagonjwa wenye pumu sugu, jambo la muhimu ni
kuepuka visababishi vya pumu na kuendelea na matumizi ya dawa zinazosaidia katika kutanua mirija ya hewa. Kwa wagonjwa wanaopata mashambulzi ya mara kwa mara wanaweza kushauriwa na daktari kutumia dawa kadhaa zikiwemo zile zinazopunguza mcharuko mwili(mast cell inhibitors, inhaled steroids au oral steroids), pamoja na dawa za
kutuliza kukakamaa kwa misuli ya mwili (muscle relaxants). Aidha ni vema pia kutibiwa na kuthibiti kutokea kwa magonjwa yote yahusuyo mfumo wa hewa. Matumizi ya chanjo ya magonjwa kama influenza na pneumococcal pneumonia nayo husaidia sana katika uthibiti wa kutokea kwa pumu. Ni vema pia kuepuka matumizi ya dawa za jamii ya beta-blockers kwa wagonjwa wenye shinikizo la damu na ambao pia wana pumu.
TIBA MBALIMBALI UNAZOWEZA TUMIA KUJITIBU PUMU UKIWA NYUMBANI
KITUNGUU THOMU
Kitunguu swaumu
Chukua punje 5 hadi 6, menya na ukate vipande vidogo vidogo lakini siyo vidogo sana na uchemshe kwenye moto na maji kikombe kimoja (robo lita), ongeza kijiko kikubwa kimoja chaasali mbichi ndani yake na uache kwenye moto kama dakika 5. Ipua na unywe kwa pamoja kutwa mara 2 hadi utakapopona.
Karafuu
Chukua karafuu 15 vitoe vichwa vyake kisha loweka hizo karafuu katika nusu gilasi ya maji usiku kucha Kunywa maji yake asubuhi kabla hujala kitu chochote. Fanya hivyo mfululizo kwa muda wa siku 15.
TANGAWIZI
Tangawizi
Tangawizi pia ina faida nyingi katika mwili wako na afya yako. Tengeneza juisi robo lita yenye mchanganyiko wa tangawizi, komamanga na asali. Kunywa mchanganyiko huo kutwa mara 2 au 3 kwa matokeo ya haraka.
Namna nyingine ni kuchukua kijiko kikubwa kimoja cha juisi ya tangawizi (majimaji ya tangawizi) changanya na kijiko kikubwa kimoja cha asali na vijiko vikubwa 2 vya mbegu kavu za uwatu na uuache mchanganyiko huu kwa usiku mmoja. Kunywa mchanganyiko huu kesho yake ili kuondoa sumu kwenye mapafu yako.
MAFUTA YA MHARADALI
Mustard Oil
Chukua mafuta kidogo ya mharadali na uchanganye na kafuri (camphor) ndani yake. Jipakae mchanganyiko huu taratibu sehemu yote ya kifua mpaka uone nafuu inajitokeza. Hakikisha unayapasha mafuta kidogo katika moto kabla ya kuanza kujipaka taratibu (masaji) ili kifua kiweze kuhisi au kulipata hilo joto na hatimaye upate uponyaji kwa aharaka zaidi. Fanya zoezi hili wiki 2 hadi 3
MTINI
Mtini ni dawa nyingine ya asili (home remedy) nzuri dhidi ya pumu. Loweka baadhi ya mitini mikavu ndani ya maji kwa usiku mmoja. Kula huo mtini uliolowekwa kesho yake asubuhi kabla ya kula kitu kingine chochote. Pia kunywa maji hayo yaliyoloweka mtini kwa ajili ya kujitibu pumu au asthma. Fanya hivi kwa wiki 2 hadi 3
MATIBABU YA PUMU CHINI YA UONGOZI WA GREEN HEALTH CONSULTATION CENTER
Mpendwa msomaji wa blog yetu hii tunakukaribisha ofisin kwetu iliyopo ilala, machinga Complex, Lindi Street Dar es salaam kwa ajili ya ushaur nasaha pamoja na matibabu ya Dawa za Asili
Matibabu ya pumu katika ofisi yetu ni matibabu ya Dawa ambazo utapatiwa kutokana na hali yako ya kiafya jinsi ilivyo
Zifuatazo ni baadhi ya Dawa zinazotumika kutibu pumu
CORDYCEPS SINENSIS CAPSULES
Dawa hii ni ya kiasili imetengenezwa kwa kutumia viambata
Cordyceps sinensis mycelium, Radix ginseng
KAZI NA FAIDA YA HII DAWA
Kuongeza kinga dhidi ya mashambulizi ya vijidudu viletavyo maradhi
Kuboresha ufanyaji kazi wa ini, mapafu na figo
Kuongeza nguvu kwa wenye matatizo ya uchovu wa muda mrefu
DAWA HII INAFAA KUTUMIWA NA
Watu wenye kinga kidogo;
Watu wenye pumu na hitilafu katika ufanyaji kazi wa maini, mapafu, au figo;
Watu wazima wenye udhaifu wa mwili
Wanariadha wanaohitaji nyongeza ya nguvu katika mwili
MAELEZO MUHIMU KUHUSU UFANYAJI KAZI WA DAWA YA CORDYCEPS SINENSIS CAPSULES
Cordyceps Sinensis imekuwa ni kitu cha thamani kwenye tiba za Asili kwa karne nyingi. Cordyceps sinensis hupatikana kwenye nyanda za juu (mita 3800 juu kutoka usawa wa bahari) za milima ya Himalaya na ni kitu kigumu sana kukivuna toka huko juu. Ugumu huo ndio ulisababisha cordyceps kuwa moja ya Dawa zenye bei ya juu sana na kuifanya itumike kwenye majumba ya kifalme na familia za kifalme Ukulima wa kisasa umewezesha dawa hii inayotokana na fungus kutoka kwenye viwavi kupatikana kwa urahisi zaidi na kuteremsha bei yake kwenye soko la dunia.
Cordyceps imebainika kuwa na uwingi wa vitu vya asili vya viumbe hai vyenye manufaa kwa binadamu kama cordyceps sinensis polysaccharide, tindikali ya cordyceps sinensis, cordycepin na adenosine, vyote vikiwa na manufaa makubwa kwa afya ya binadamu. Baadhi ya manufaa hayo ya cordyceps ni:
KUONGEZA KINGA :
Hufanya kazi vizuri sana ikiambatanishwa na Ginseng, vidonge vya cordyceps plus huimarisha kinga za mwili na kuusaidia mwili kuhimili mashambulizi ya vijidudu vya magonjwa kama bakteria, virusi na viumbe wengine tegemezi (parasites).
KUTIBU PUMU NA KUIMARISHA NA KUBORESHA MFUMO WA UPUMUAJI:
Cordyceps hutibu pumu na huimarisha mfumo wa upumuaji kwa kuilegeza misuli (relaxing the bronchial smooth muscles) laini ya njia za hewa za kwenye mapafu. Inasaidia kikohozi cha muda mrefu (chronic cough), magonjwa yanaoshambulia ngozi nyororo inayotanda juu ya njia za hewa za mapafu (bronchitis), TB ya mapafu (pulmonary tuberculosis), ugonjwa wa chronic obstructive pulmonary disease (COPD), na pumu (asthma).
KUTIBU NA KUIMARISHA FIGO.:
Tafiti zimeonyesha kuwa cordyceps ina uwezo mkubwa wa kuboresha ufanyaji kazi wa figo na kinga za mwili za wagonjwa wenywe matatizo kwenye figo zao.
KUTIBU NA KUIMARISHA MAINI:
Karibu katika tafiti zote za tiba cordyceps imeonyesha kuimarisha ufanisi katika ufanyaji kazi wa ini. Katika bara la Asia, cordyceps imetambuliwa kuwa ni tiba ya kutumia mimea kwa kuponya matatizo ya muda mrefu ya magonjwa ya ini ya hepatitis B na C.
GANODERMA CAPSULES
Dawa hii ni ya kiasili imetengenezwa kwa kutumia viambata ambavyo ni Ganoderma, Cordyceps Sinensis Mycelium, Radix Ginseng
KAZI NA FAIDA YA HII DAWA
Kuboresha kinga za mwili na hivyo kuzuia kansa
Kupunguza madhara yatokanayo na tiba za mionzi na chemotherapy (kama kutapika, maumivu, upungufu wa chembechembe nyeupe za damu, kutoota nywele, uchovu, n.k.)
kuongeza kasi ya uponyaji baada ya tiba za mionzi na chemotherapy
Kuongeza kinga za mwili
kupunguza makali ya brochitis sugu, pumu na mzio.
DAWA HII INAFAA KUTUMIWA NA
Watu wanohitaji kuongeza kinga za mwili
Watu wenye uvimbe usio na madhara (benign tumor) na uvimbe wenye madhara (malignant tumor).
watu waliomaiza tiba za chemotherapy na radiotherapy
Watu wagonjwa au walio kwenye uangalizi wa kitiba
Watu wenye brochitis sugu, pumu, mzio au matatizo mengine ya mfumo wa upumuaji
UFANYAJI KAZI WA GANODERMA CAPSULES KAMA DAWA YENYE FAIDA NA NGUVU NYINGI
KUONGEZA KINGA MWILINI:
Katika kitabu cha Compendium Of Materia Medica, ganoderma imeitwa nyasi za kimiujiza, "Supernatural grass". Ganoderma ina ganoderma amylose, triterpenoids za ganoderma lucidum, alkaloid na amino acids 17, germanium asilia, selenium asilia na elementi nyingine adimu
Ganoderma inapendekezwa kuwa ni kitu cha kuongeza kinga za mwili kwa muda mrefu.
KUZUIA SARATANI:
Utendaji kazi wa ganoderma spore ni mara 80 zaidi ya ule wa ganoderma. Ganoderma spore inaweza kuimarisha kinga za mwili za seli, na hivyo kuziwezesha kurudia hali ya kawaida baada ya tiba ya mionzi, tiba ya chemotherapy au upasuaji.
KUTIBU PUMU NA KULINDA MAINI:
Mchanganyiko wa ganoderma, cordyceps na ginseng hufanya kazi vizuri katika kutibu pumu na kulilinda ini. Ina uwezo wa kupunguza SGOT na SGPT (vimeng'enya vya ini ambavyo ni ishara ya matatizo katika ini). Kwa kulisaidia ini, kasi ya uvunjwaji wa cholesterol huongezeka na kupunguza kiwango cha cholesterol katika damu.
AFYA YA MOYO NA MISHIPA YA MOYO:
Ganoderma huzuia kujikusanya kwa platelet katika damu hivyo kuboresha mtiririko wa damu. Inaboresha pia uchukuliwaji wa oksijeni katika damu na hivyo kuongeza matumizi ya oksijeni kwenye viungo vya mwili, kama moyo na ubongo.
KUDING TEA
Hii ni chai ya kiasili ambayo imetengenezwa kwa kutumia viambata ambavyo ni Folium Ilicis Kudingchae, Radix Panacis Quinquefilii, Ganoderma, Folium Camelia
KAZI NA FAIDA ZA CHAI HII
Kuding tea ina kazi nyingi mwili ambazo ni
Kuzuia mafua ya mara kwa mara Inazuia rhinitis, kuwashwa kwa macho, macho mekundu na maumivu ya macho yanayotokana na joto
Hutibu pumu
Kutoa sumu na kusaidia kutembea kwa chakula tumboni
Inasaidia kutuliza akili na kumbukumbu
Inasaidia kurahisisha mzunguko wa damu hupunguza cholesterol, sukari katika damu na pressure
Inazuia kuzorota kwa ufanyaji kazi wa moyo na ubongo
Inauweka mwili kwenye uzito unaofaa
Huimarisha mfumo wa upumuaji
Chai ya kuding tea inatumika na Makundi yote isipokuwa wanawake wenye mimba
THAMANI YA LISHE YA KUDING TEA:
Kuding Tea ina uwingi wa kuding saponin, american ginseng saponin ambazo zimepewa majina ya kudinosides na kudinlactones; pia ina ganoderma lucidum polysaccharide, polyphenols, flavonoids, quercetin, selenium, vitamini C,D,E na madini. Kiwango cha flavonoids ndani ya kuding tea ni zaidi ya mara 10 ya kile kilichimo ndani ya majani ya chai ya aina nyingine.
FAIDA ZA KIAFYA ZA KUDING TEA:
Utafiti wa hivi karibuni unaonyesha kuwa kuding tea inasaidia mzunguko wa damu mwilini, inapunguza pressure,inaondoa kukauka kwa koo, stomatitis, gingivitis, inapunguza lipids kwenye damu, ikiwa ni pamoja na cholesterol. Ina sifa ya kuzuia kudhoofika kwa utendaji kazi wa moyo na ubongo na kuuweka mwili katika uzito unaotakiwa. Inapendekezwa kwa matatizo ya ini kuwa na mafuta (fatty liver) na kukosa choo. Kiwango cha kutosha cha faida za mwili kinahusishwa na kuding. Inasadidkika kuwa inaondoa hali ya kutotulia, na kiu hasa mtu anapokuwa anaumwa ugonjwa ambao unampa homa kali au kuharisha. Inaondoa kikohozi na kutibu bronchitis. Mwisho, inasadikika kuwa kuding tea inaongeza kasi ya mmeng'enyo wa chakula na kuboresha utulivu wa mawazo na kumbukumbu.
TABIA ZA KIPEKEE ZA CHAI YA KUDING TEA
Utakapokunywa kuding tea kwa mara ya kwanza utaiona kuwa si ya kwaida. Ina ladha kamili, yenye uchungu, ambayo kwanza itakufanya usiipende. Lakini kwa chini ina utamu fulani, utamu ambao unaongezeka pale ambapo uchungu unapoisha
Share:

Related Posts: